ad

ad

Zari atangaza kuachana na Diamond


Zarinah Hassan maarufu kama Zari ama Zari The Boss Lady ametangaza kuachana na mzazi mwenzake, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kufuatia kuwapo kwa tuhuma nyingi kuhusu mwanamuziki huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengine.

Zari ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa kumekuwapo na tuhuma na wakati mwingine kuna uthibitisho katika mitandao kuhusu tabia ya mara kwa mara ya Diamond kuchepuka, na hivyo ameamua kuachana na kwa sababu heshima yake, utu wake haviwezi kuharibiwa.

Zairi amesema kwamba anaachana na Diamond kama mpenzi wake lakini wataendeleaa kuwa wazazi wenza.

Aidha, katika waraka wake, Boss Lady amesema kuwa, tukio hilo halitapunguza namna anavyowajali wanae, na Zari ambaye amekuwa akifahamika kwa kujituma siku zote.

Zari ametangaza uamuzi wa kuachana na Diamond jana wakati watu wakisherehea siku ya wapendanao, ambapo wengi wameigeuza na kuwa siku ya wapenzi ambapo kila mmoja anajaribu kumuonyesha mwenzake namna anavyompenda kwa kufanya mambo mbalimbali.

Zari ameandika;
Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised.

We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know.

I will continue to build as a mogul, i will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters.

HAPPY VALENTINE’S.

No comments

Powered by Blogger.