Paul Pogba akishangilia na Jesse Ellis Lingard katika moja ya mechi ya Ligi Kuu.
Mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye muda wowote kuanzia sasa anatarajiwa
kujiunga na Man United akitokea Arsenal, ametajwa kuwa ndiye mchezaji
atakayekuwa akilipwa mkwanja mrefu zaidi kikosini humo akimuacha kwa
mbali kiungo, Paul Pogba.
Mtandao
maarufu ambao unaaminika kwa habari za usajili Ulaya umeweka wazi kuwa
Sanchez atakuwa akilipwa £450,000 kwa wiki ukiwa ni mshahara mkubwa kwa
wachezaji wanaocheza Premier League. Angalia listi ya wachezaji wengine
na Man U wanaomfuatia Sanchez kwa kupokea mishahara mikubwa.
1. Alexis Sanchez – £450,000
2. Paul Pogba – £260,000
3. Romelu Lukaku – £220,000
4. David de Gea – £200,000
5. Zlatan Ibrahimovic – £150,000
6. Juan Mata – £145,000
7. Nemanja Matic – £140,000
8. Henrikh Mkhitaryan – £140,000
9. Marouane Fellaini – £120,000
10. Chris Smalling – £120,000
Post a Comment