HANS POPPE AMPA GARI SAID NDEMLA
Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla.
Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, leo.
Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa
inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla
alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante
Kwasi.
Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla.
“Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema
nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona
Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,”
alisema.
“Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu
wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na
kuisaidia timu.”
Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji
wa Simba. Alianza na Hussein Zimbwe aliyempa gari aina ya Toyota Raum.
Lakini akaonyesha gari aina ya Toyota Lactic na kusema atapewa mchezaji
atakayefanya vizuri.
Kuhusiana na aina, leo amesema: “Aina utaijua baadaye ila gari haiko mbali. Hivyo tutaangalia siku yenye nafasi atakabidhiwa.”
Post a Comment