Maelekezo ya Bodi ya Mikopo kwa wadaiwa ambao bado hawajaajiriwa
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanufaika wote
wa mikopo ambao wanadaiwa na hawajaajiriwa bado, wafike katika ofisi za
bodi hiyo zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini ama kuwasiliana nao,
ili wapewe maelekezo na utaratibu maalum wa namna ya kulipa mikopo yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizoko Mwenge,
Jijini Dar es Salaam, mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru ametoa wito kwa wale ambao
bado hawajaanza kurejesha mikopo yao, hata kama bado hawajapata ajira
maalumu, wafike katika ofisi za bodi maeneo mbalimbali nchini ili kupewa
maelekezo na utaratibu wa namna ya kuanza kurejesja mikopo hiyo.
“Tunatoa
wito kwa wale ambao kwa sababu fulani fulani walikuwa hawajaanza
kulipa, walipe na wanakaribishwa kwenye ofisi zetu. Hata wale ambao
hawako kwenye ajira maalum kuna utaratibu maalum tumewatengenezea.
Wanaweza kuwasiliana na sisi katika mawasiliano yetu au wakaja ktika
ofisi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na kwingineko
il tuwape maelekezo na utaratibu maalum wa kulipa.” amesema Mkurugenzi
Badru
Aidha
Mkurugenzi Badru amesisitiza kuwa Bodi itahakikisha kuwa
inawashughulikia wale wote ambao bado hawajarejesha mikopo yao ili
waweze kuirejesha ikiwemo kuwachukulia hatua za kisheria na kuwafikisha
mahakamani.
“Mtu
yeyote aliyekopa mkopo kwa ajili ya kusoma, njia pekee ya kisheria
inayoweza kumfanya asilipe mkopo huu, ni labda awe amefariki. Lakini
kama umekopa, uko hai, uko hapa nchini na hata ukienda nje, sisi ni
lazima utalipa huo mkopo kwa gharama yoyote ile,” amesisitiza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji wa Mikopo, Phidelis Joseph
amewataka wale ambao tayari wameshaanza kurejesha madeni katika akaunti
za benki za Bodi ya Mikopo, waweke maelezo yote katika ”pay-in-slip’
zao.
“Wale
wanufaika ambao wanajitokeza na wanalipa kwenye zile ‘bank accounts’
zetu waweke ‘details’ zote. ‘Unapodeposit’ unatakiwa utoe taarifa kwa
Bodi ya Mikopo kwamba nimeweka pesa. Lakini vie vile unapoiandika ile
‘slip’ yako uiandike vizuri..,” amesema Phidelis Joseph.
Vile
vile amewataka wanufaika wa mikopo ambao wameshaanza kulipa, wafike
katika ofisi za Bodi ya mikopo ama kutumia mitandao ya Bodi, kwaajili ya
uhakiki.
Post a Comment