Bodi ya Mikopo (HESLB) Yawageukia Waajiri
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema kuanzia
Jumatatu ijayo, Januari 8, 2018 itaanza kukagua taarifa za mishahara za
waajiri (payroll) ili kubaini waajiri ambao wanawasilisha kiwango kidogo
cha mikopo ya wafanyakazi wao ambao ni wanufaika pamoja na waajiri
ambao hawawasilishi kabisa pesa hizo kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa
sheria ili wachukuliwe hatua stahiki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema wanufaika wengi wa
mikopo, wakiwemo wadaiwa sugu, wameonesha ushirikiano mkubwa katika
kurejesha mikopo yao, hivyo kurahisisha kazi ya kukusanya madeni ya
mikopo hiyo.
“Kiasi
cha pesa za wadaiwa sugu kilichoiva na kinachotakiwa kuwasilishwa ni
Tsh. bilioni 285, hii inajumuisha kuanzia kazi hii ya kukopesha
ilipoanza.
“Tangu
mwaka jana mpaka sasa tumewapata wadaiwa sugu 26,000, tunashukuru
wanufaika hawa wamejitokeza na wanawasilisha mikopo yao. Kuna baadhi ya
waajiri wanawasilisha vizuri marejesho ya wanufaika wa mikopo ya elimu
ya juu, wengine hawasilishi na wengine wanawasilisha kiasi kidogo
tofauti na asilimia 15 kama sheria inavyotamka.
“Kuanzia
Jumatatu, Jan. 8, 2017 tutaanza kukagua taarifa kwenye payroll za
waajiri wote waliosajiriwa kubaini waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa
mikopo wanaodaiwa ili waweze kukatwa.
“Lengo
la kufanya ukaguzi kwenye payroll za waajiri ni kubaini iwapo wana
waajiriwa wanadaiwa na HESLB, waajiri wanaowasilisha kiwango
kinachotakiwa, wanaowasilisha chini ya asilimia 15 na wanaokata pesa na
hawaziwasilishi HESLB,” alisema Badru.
Hata
hivyo, Badru amesema wamelazimika kufungua ofisi zao nchi nzima kwa
ajili kusimamia malipo ya fedha hizo za mikopo, hasa wale waliotajwa
kwenye orodha ya wadaiwa sugu ambapo wamewasambaza wakaguzi nchi nzima,
kwa ajili ya kufuatilia waajiri wasiotekeleza wajibu wao wa kuwakata
asilimia 15 wanufaika hao waliowaajiri.
Post a Comment