Jibu la Polisi baada ya kuagizwa na Waziri kuwakamata watuhumiwa ndani ya siku 7
Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa amesema polisi wanafanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Jeshi hilo.
Juzi,
Kigwangalla mbali na kutoa agizo hilo, amesema watu hao wanne pia
walipanga njama za kumuua mwanaharakati, Wayne Lotter na kwamba polisi
wakishindwa kuwakamata atawashtaki kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwakalukwa
amesema jukumu lao ni kukamata wanapopata shitaka la kuwapo kwa kitu
kisicho cha kawaida, kuchunguza na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP) kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine.
“Kazi
yetu ni kukamata, kuchunguza na kupeleka kwa DPP kwa ajili ya taratibu
nyingine, hatufanyi kazi kwa matamko ya bungeni,” amesema na kuongeza;
“Alichokisema
mheshimiwa Kigwangalla nimekisoma kwenye vyombo vya habari akihusisha
na suala la mwanaharakati aliyeuawa, sisi hatufanyi kazi kwa kufuata
vyombo vya habari vimeandika nini au limetolewa tamko gani au kuna
shinikizo gani, tunafanya kwa kufuata taratibu zilizopo.”
Post a Comment