Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB)
Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo:
• Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz
• Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha.
• Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020
• Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet”
• Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe.
• Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka.
• Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150
• Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 26/01/2018
Post a Comment