WANAWAKE WASAGANAJI WA GHANA WAOANA UHOLANZI
KINYUME na matarajio na utamaduni wa Afrika, ndoa za jinsia moja ambazo ni jambo linaloshutumiwa kwa kiwango kikubwa barani Afrika, zinaonekana kuwanyemelea watu wa bara hili.
Pamoja na kupingwa karibu sehemu zote, tabia hiyo ambayo imeenea rasmi na au kwa kificho sehemu nyingi duniani, imeanza kuwa tishio la kuvuruga mifumo ya mila na tamaduni za asili za binadamu katika misingi ya kawaida ya kijamii, kidini na kimaumbile.
Katika tukio la hivi karibuni nchini Uholanzi, wanawake wawili waliosemekana kuwa ni wananchi wa Ghana, walifunga ndoa kwa kivuli cha mume na mke. Tukio hilo lilinaswa na vyombo mbalimbali vya habari vikiwaonyesha wanawake hao wakiwa katika mavazi ya harusi; mmoja akiwa amevaa mavazi ya kiume na mwingine mavazi ya kike.
Katika mazingira ambayo hayakufahamika, majina ya wanandoa hao, hayakutajwa licha ya sura zao kuonyeshwa waziwazi.
Picha nyingine, miongoni mwa nyingi zilizonaswa ni ile wanayobusiana kuonyesha penzi lao, wakiwa wamevaa nguo zenye asili na mapambo ya Ghana.
Pamoja na tukio hilo kushutumiwa na baadhi ya watu wa Ghana, kuna uwezekano wa kuwepo au kuendelezwa kwa mjadala kuhusu ndoa za jinsia moja nchini humo.
Kwa mujibu wa Rais wa Ghana, Akufo Addo, akihojiwa na kituo cha Al Jazeera, nchi yake inaweza kuhalalisha ndoa za jinsia moja iwapo patakuwa na matakwa mengi ya kufanya hivyo.
Moja ya baadhi za picha walizopigwa wanandoa hao ambapo majina yao hayakutajwa kwa sababu zisizojulikana.
Post a Comment