Taarifa ya serikali kuhusu kuzimwa kwa 'chaneli' za bure kwenye ving'amuzi
Kufuatia
uwepo wa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa
huduma ya runinga za bure pindi vifurushi katika visimbusi (ving’amuzi)
vyao vinapomalizika, serikali imetolea ufafanuzi suala hilo kwa kueleza
namna mfumo wa utendaji unavyotakiwa kufanya kazi.
Akijibu
maswali ya watumiaji mbalimbali wa mtandao wa Twitter kuhusu urushwaji
wa runinga za bure, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Abbas alisema, kwa
mujibu wa sheria iliyopo sasa, vituo vyote vya runinga ambavyo vimepewa
leseni ya FTA (Free to Air) vinapaswa kuonekana hata baada ya kifurushi
kwenye kisimbusi kwisha.
Dkt.
Abbas alisema kwamba, hadi sasa kuna vituo 16 vya runinga vya ndani ya
nchi vilivyopewa leseni hizo, vikiwemo vituo vya ITV, Clouds TV na
Channel 10.
Aidha,
alifafanua kuwa, ili mtumiaji aweze kutazama hata baada ya kufurushi
chake cha malipo kwisha, kituo cha runinga (mfano ITV) kinapaswa
kuwalipa warushaji wa masafa (mfano Azam) ili ITV iweze kuonekana kwa
wananchi hata ambao hawajalipia visimbusi vyao.
“…
mfumo uko hivi: ili wewe uone bure hizo channeli kuna mzalishaji wa
vipindi ambaye ni kituo cha TV na msafirisha masafa mfano StarMedia. Ili
wewe uone bure kuna gharama huyo wa kwanza anatakiwa kulipia kwa wa
pili. Asipolipia akakatiwa huduma hautaona. Kwa sasa ndio mfumo.”
Pia,
Dkt. Abbas alitahadharisha kuwa, endapo kituo cha runinga hakutawalipa
wasafirishaji wa masafa, watakatiwa huduma na hivyo kuwafanya wananchi
washindwe kuweza kutazama runinga bure.
Kuhusu
TBC kuonekana katika visimbusi vyote hata bila malipo, msemaji
alifafanua kuwa, kila kisimbusi kinatakiwa kuweka TBC kupitia sera ya
‘must carry’ ambayo inaiwezesha kuonekana kwa wananchi bila malipo
yoyote.
“Unapata
TBC mda wote kwa sababu TBC anahadhi inayoitwa “must carry” ambaye
mrusha masafa yeyote Tz lazima aioneshe TBC. Kama hupati channeli
zingine za FTA muulize mtoa huduma wako. Majibu atakayokupa nijulishe na
unipe jina la mtoa huduma wako,” aliandika Dkt. Abbas.
Alisema
kuwa, kwa sasa serikali haina mfumo wa kuwaadhibu wamiliki wa vituo vya
runinga wenye leseni za FTA lakini hawawalipi warusha masafa ili
wananchi waweze kuona runinga hizo bure, badala yake, warusha matangazo
hayo wanatawakati huduma kama hawajalipwa.
“…kwa kanuni iliyoanza Machi mwaka huu, mtoa huduma za TV asipolipa kwa msafirisha masafa anaweza kukatiwa huduma.”
Kuhusu
Dstv na Azam kukata matangazo ya runinga za ndani baada ya kifurushi
kwisha, Dkt Abbas alisema suala hilo lipo Baraza la Ushindani hivyo
wananchi wasubirie majibu, na kwamba asingependa kulizungumzia kwa sasa.
Post a Comment