CHAMA CHA WASAMBAZAJI FILAMU TANZANIA WASITISHA KUKUNUNUA STIKA ZA TRA
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za Kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za Kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
Mwenyekiti wa kikosi kazi
kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Moses Mwanyilu
akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofaa
kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini
huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu
ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za
kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa.
Mjumbe wa chama cha wasambazaji
wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja
waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao
kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha
suala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala
kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na
kujadiliana kuhusu swala hili.
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na
waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao
bodi ya filamu Tanzania kwa ajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu
kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za
nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na
sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA
wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika
huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya
filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani
zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.
Post a Comment