ad

ad

Sanchi Awavimbia Kichwa Polisi Kisa Nguo Fupi

  Mrembo Jane Rimoy maarufu kama Sanchoka au Sanchi.


WAKATI Rais John Pombe Magufuli akiziagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisha maadili ya Kitanzania yanalindwa kwa kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wake, mrembo Jane Rimoy maarufu kama Sanchoka au Sanchi anaonekana kuwavimbia kichwa Polisi baada ya kuendelea kuposti picha zake akiwa nusu utupu.

Akillihutubia taifa wakati wa sherehe za kumbukumbu ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara mjini Dodoma Desemba 9 mwaka huu, Rais Magufuli alizitaka mamlaka zinazohusika na makosa ya mitandao, kuwachukulia hatua mara moja watu wanaokiuka maadili, huku akitoa onyo kwa wasanii na watu wengine wanaovaa nusu utupu.
Lakini akiendelea kutupia picha hizo, Sanchi ameliambia Risasi Mchanganyiko kuwa hawezi kubadili aina ya mavazi anayovaa kwa kuwa hayakiuki maadili.
Sanchi alisema ataendelea kuvaa mavazi yake aliyozoea kila siku kwa vile anajua havinji sheria maana ni mazuri na hayana shida.

“Mimi naendelea kuvaa mavazi yangu kwa sababu toka zamani ndiyo navaa hivi na ninajua wazi sio mlengwa wa hiyo kauli ya mkuu, halafu mimi pia ni mwanamitindo, ni lazima nibuni mtindo wangu,” alisema.
 
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo, alisema jambo hilo bado halijafika mezani kwake, lakini anaamini vijana wake watalifanyia kazi mara moja, kwa kuwa wapo hapo kwa ajili ya kuhakikisha sheria inafuatwa.

“Kazi inafanyika kwa watu wote wanaotumia mitandao vibaya, siyo Sanchi tu bali wasanii wengine pia, tupo hapa kuhakikisha agizo la rais linatekelezwa na hakuna mtu atakayeachwa, hilo ndilo ninaloweza kusema kwa sasa,” alisema Kamanda Murilo.

CHANZO: GPL

No comments

Powered by Blogger.