ad

ad

Masailand: Hoteli Nzuri Ya Kitalii Arusha!


Mwonekano wa mbele wa Hoteli ya Masailand.

Taswira mbalimbali za hoteli hiyo.

Mwonekano wa vitanda.
Sundown inavyoonekana ukiwa ndani ya Hoteli ya Masailand.



Sehemu ya meza za mikutano katika Hoteli ya Masailand.
UKIZUNGUMZIA Mkoa wa Arusha na vivutio vyake, kamwe huwezi kuiweka pembeni Hoteli ya Masailand yenye mandhari nzuri kwa mapumziko.
Akiizungumzia hoteli hiyo ya kisasa, afisa uhusiano wa hoteli hiyo, Johari Chuo alisema hoteli hiyo ya kisasa ina zaidi ya vyumba 54 vyenye hadhi ya kimataifa na kumbi za mikutano na harusi zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 600 hadi 700 na kila mahali kukiwa na kiyoyozi (AC).
Alisema raha zaidi katika hoteli hiyo ni kwamba, kipupwe hicho unajipia mwenyewe kulingana na mahitaji yako. Unaweza pia kuweka joto kama hupendi baridi.

Kama hiyo haitoshi, Johari alisema katika hoteli hiyo kuna migahawa ya ndani na ya nje na kuna ‘swimming pool’ ambapo wageni mbalimbali wanakaribishwa kujionea utofauti wa hoteli hiyo na nyingine zote Arusha.
Aidha, kwa wale wapenda mazoezi, hoteli hiyo imewathamini kwa kuweka sehemu maalum ya kufanyia mazoezi ya mwili (gym).

“Vyumba vyetu ni safi na vyenye kuvutia kwa mteja awapo ndani kwani anaweza kuona vivutio mbalimbali vya mkoa wa Arusha kama vile Mount Meru, Sundown na Kisongo Valley.
“Mteja wetu ana uwezo wa kubadilisha kiyoyozi kadri hali ya hewa inavyobadilika kama akihitaji hali ya ubaridi atawekewa na hata hali ya joto, nawasihi wateja wafike kwa wingi katika hoteli yetu,” alisema.
Afisa uhusiano huyo alisema, mbali na sehemu ya vyumba vya kulala wageni, kuna baa kwa ajili ya wageni mbalimbali.

KWA MAWASILIANO ZAIDI:

PHONE NO: +255 624722020
EMAIL ADDRESS: marketing@masailandsafari.com

No comments

Powered by Blogger.