ad

ad

Hiki Ndicho Alichokizungumza Zari Kabla ya Kuonekana na Diamond (Video)

SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars Mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zari mchana wa jana Jumamosi alisimamisha shughuli katika maduka yaliyopo Mlimani City alipokwenda kuzindua duka jipya la samani, Danube. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika kufanya manunuzi katika maduka hayo walijazana nje ya duka jipya la Danube wakitaka kumuona Zari huku wakiimba wifi... wifi. Purukushani zilitawala nje ya duka hilo wakati kila mmoja akijaribu kumsukuma mwenzake ili aweze kumuona Zari aliyekuwa ameketi katika makochi akizungumza na wafanyakazi. 
SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars Watu walivutiwa kumuona mwanamke huyo kutokana na hivi karibuni kupamba vichwa vya habari baada ya Diamond kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto. Ujio wa Zari nchini amekuwa na mvuto kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakilinganisha matukio katika maisha ya Diamond, Zari na Hamisa.

No comments

Powered by Blogger.