Acacia Wasema hawana Dola Milioni 300 za kuilipa Serikali ya Tanzania kama ilivyokubaliwa katika mazungumzo
Kampuni
ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa
haina uwezo wa kulipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Akiongea
jana Oktoba 20, 2017 kwa njia ya simu na chombo cha habari cha
Kimataifa cha Uingereza (Reuters) Afisa wa Fedha wa Acacia, Andrew Wray
kampuni hiyo haina uwezo wa kulipa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania.
Washirika
wakubwa wa Acacia, Barrick Gold siku ya juzi Oktoba 19 walikubalina na
serikali ya Tanzania kuwa watalipa dollar milioni 300 kwa serikali ya
Tanzania pamoja na kugawana mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji
wa madini nchini.
Post a Comment