Zitto Kabwe Aitupia Lawama Serikali Baada ya Acacia Kusema Hawana hizo Dola Milioni 300 za Kuilipa Tanzania
Baada
ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina pesa
za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa juzi na kampuni ya
Barrick Gold Mining, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na
kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.
Akifanya
mahojiano maalalumu jana mchana, Mh. Kabwe alisema kwamba alitegemea
kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya
kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika
uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha
ya kodi waliahidi hivyo.
Mh.
Zitto amesema kwamba tangu juzi alishangaa sana kusikia serikali
ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya
Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya
Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama
yenyewe.
"Nilitegemea
hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa
tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo
waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa
kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na
walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa
sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".
Kampuni
ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa
haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Post a Comment