ad

ad

Wasanii, Viongozi Wasifu Uamuzi Wa Diamond


Dar es Salaam. Baadhi ya wasanii pamoja na viongozi nchini wametoa yaliyomo mioyoni baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuzungumza leo kuhusu uhusiano wake.
Baada ya msanii huyo kukiri kuwa amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto, baadhi ya wasanii maarufu pamoja na viongozi wameonyesha kumuunga mkono Diamond kutokana na kueleza ukweli.

“Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana, kwani uwezo wako wa kupitia kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima,” maneno yaliyoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ameweka picha ya mwanadada Zari.

Zari ni mama wa watoto wawili wa Diamond ambaye anaishi naye kwa sasa.
Pia Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule maarufu kama Profesa J ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter akisema ukweli humweka mtu huru kweli kweli huku akiwa ameweka picha ya Diamond Platnumz.

Si hao tu waliofunguka kueleza hilo bali hata Haji S Manara ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba amempongeza Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuzungumza kiume.

Kwa upande wake Soggy Doggy Hunter amempongeza Diamond kwa kuongea yote na kuwa muwazi na kumuombea Mungu amsimamie.
Mkude Simba amenukuu maneno ya msanii huyo aliyosema “Mwanamke yeyote mwenye mtoto wangu na amlete siwezi kukataa damu kama kweli ni mtoto wangu.”

No comments

Powered by Blogger.