TIGO FIESTA KUKINUKISHA ARUSHA JUMAMOSI IJAYO, UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID
Tamasha la Tigo Fiesta
linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid, Arusha huku wasanii kibao wakitajwa kusajiliwa kutoa burudani kwenye
tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika karibu nchi nzima.
Akizungumza na Wanahabari
kwenye Makao Makuu ya ofisi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, William Mpinga alisema
katika tamasha hilo wasanii pendwa zaidi ya 17 tayari wameshasajiliwa akiwemo
Alikiba Christian Bella, Shilole, Saida Karoli, Mr Blue, John Makini na wengineo.
Mpinga amesema kuwa wateja
watakao taka kwenda kwenye tamasha hili wataweza kununu tiketi za kiingilio kwa
Tigo Pesa kupitia namba 0678888888 ambapo mteja yeye atakayenunua tiketi kwa
kutumia huduma hiyo atapata pinguzo la asilimia 10.
Post a Comment