Maalim Seif Amtembelea Tundu Lissu Nairobi Kenya
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad Septemba 26,
2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa
Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS),
Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.
Mwenyekiti
wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na
kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini
Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.
"Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini
Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye amelazwa
Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro
Mhe. Shariff Hamad ameongozana na Mhe. Juma Duni Haji Nairobi kumjulia hali, Mhe Tundu Lissu.
Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa
nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
Post a Comment