Basi La Tashriff Lateketea Kwa Moto Likitoka Tanga Kwenda Dar
Abiria
waliokuwa wakisafiri kutoka Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam
wamenusurika kufa baada ya basi walilokuwa wamepanda la kampuni ya
Tashriff kuteketea kwa moto.
Kwa mujibu habari ambazo zimepatikana na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba zimedai kwamba ajali hiyo imetokea saa nane machana katika eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamesema wameona moshi ukitoka chini ya basi
hilo ndipo wakapiga kelele na kusababisha dereva kusimama dakika chache
baada ya hapo likaanza kuwaka moto.
"Tumesikia
kelele kutoka kwa watu waliokuwa nje tukaona dereva kasimamisha basi
muda si mrefu moshi ulianza kutoka mara moto ukalipuka"amesema Bahati
Mussa abiria wa basi hilo.
Kamanda
Wakulyamba amesema basi hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Hemed Ali
(35) lilikuwa na abiria 29 ambapo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza
maisha.
"Hakuna
aliyejeuhiwa wala kupoteza maisha imeteketea kwa moto"amesema
Wakulyamba na kusisitiza kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi
kujua chanzo cha moto huo
Post a Comment