Kiongozi wa Upiinzani Uganda Kakamatwa kwa Kuhamasiha Wananchi Kupinga Kufutwa kwa Ukomo wa Rais
Kiongozi
mkuu wa chama cha Former Forum for Democratic Change (FDC) Dk Kizza
Besigye amekamatwa leo saa moja kabla ya Bunge kuanza kujadili pendekezo
la kuondoa ukomo wa umri wa rais.
Besigye,
aliyewahi kugombea urais mara nne na akishindwa kwa Rais Yoweri
Museveni alikamatwa mjini hapa alipokwenda kuwahamasisha wafuasi wake
kupinga kufutwa Ibara ya 102 (b) kwenye Katiba iliyoweka ukomo wa
kugombea urais kuwa miaka 75.
Besigye
alikataa kushuka kutoka kwenye gari lake hali iliyowalazimisha maofisa
wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kampala (DPC) wakiongozwa na Joseph
Bakaleke kulivuta gari lake hadi kituoni hapo.
Vilevile
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Fred Mukasa Mbidde alikamatwa
kuhusiana na suala hilo hilo. Zilikuwepo taarifa za kukamatwa vijana
wengi katika maeneo mbalimbali yalikofanyika maandamano ya kupinga
pendekezo hilo. Maeneo mengine yalikofanyika maandamano ni Mbale, Arua,
Mbarara, Masaka na Pader
Katika
hatua nyingine, maofisa polisi walisambazwa katika maeneo mengi muhimu
katika jiji la Kampala ulinzi unaohusiana na pendekezo la kufutwa Ibara
ya 102 (b) ya Katiba likilenga kuondoa ukomo wa umri wa rais.
Makao
makuu ya ofisi za chama cha FDC yalizingirwa na polisi wa kawaida, wa
kuzuia ghasia na wa kupambana na ugaidi. Ofisi hizo zilizopo
Najjanankumbi katika barabara ya Kampala-Entebbe zimezungukwa na polisi
wenye silaha.
Msemaji
wa Polisi Asan Kasingye alisema juzi kwamba maofisa hao wamesambazwa
kwa ajili ya kukabiliana na kitisho cha aina yoyote. Kadhalika maeneo
mengi nyeti, eneo lililojaa shughuli za kibiashara na Bunge yote
yanalindwa.
Polisi
wa kijeshi pia wamesambazwa maeneo ya Constitution Square ambako
wameweka mahema sawa na bungeni, eneo muhimu kwa ajili ya mjadala
uliotarajiwa kuwasilishwa jana kuhusu kuondolewa ukomo wa umri.
Kusambazwa
kwa wingi kwa askari hao kumefanyika katikati ya kampeni zinazofanywa
na za vikundi vya kisiasa na sasi za kiraia kupinga marekebisho ya
katiba yanayolenga kufuta ukomo wa umri wa rais wa miaka 75. Hoja ya
marekebisho hayo ilitarajiwa kuwasilishwa jana baada ya kushindikana
Alhamisi iliyopita.
Mjadala
ni mkali ndani ya bunge na chama tawala cha NRM wakiwemo baadhi ya
wenyeviti wa majimbo ambao wamepinga pendekezo la kufuta Ibara ya 102
(b) ya Katiba wakisema ni jaribio la kupindua sheria mama.
Baraza
la Viongozi wa Dini nchini limeongeza uzito kwa kutoa wito kwa serikali
kuruhusu hoja ya ukomo wa umri wa rais iamuliwe na wananchi wote kwa
kupiga Kura ya Maoni.
Baraza
hilo linalojumuisha wakuu saba wa madhehebu makubwa ya dini nchini
limesema katika taarifa yao ya pamoja wiki iliyopita kwamba watu
waruhusiwe kuamua hatima yao.
“Mjadala
kuhusu kuondolewa kwa ukomo wa umri wa rais si suala la upande mmoja
ambalo linahodhiwa na wanasiasa na au wabunge...wananchi wana maoni
tofauti kuhusu sauala hilo, hivyo kuna haja ya kusikiliza kwa utulivu
pande zote bila ya kuegemea upande mmoja na kuutisha mwingine.
Hivi
karibuni wabunge wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM)
na wa kujitegemea walipitisha uamuzi wa kuondolewa ukomo wa umri wa
miaka 75 uliowekwa katika Katiba.
Ikiwa
marekebisho hayo yatapitishwa bungeni, itakuwa na maana kwamba Rais
Museveni mwenye umri wa miaka 73 sasa ataweza kugombea uchaguzi ujao
mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 77. Mwaka 2005, katiba ilifanyiwa
marekebisho ukaondolewa ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano kila
mmoja
Post a Comment