Kumbe Ruby Alikuwa na Ujauzito Feki?
BAADA ya hivi karibuni kuonekana na
mwenyewe kukiri kwamba ni mjamzito lakini ghafla ujauzito huo kuyeyuka
na kuzua gumzo kwa mashabiki wake, msaniii wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ kumbe alidanganya mashabiki.
Akifungukia ujauzito huo katika mahojiano maalum na Risasi Jumamosi, Ruby alisema kuwa anakumbuka miezi kadhaa iliyopita alienda kwa mama yake akampikia chakula aina ya pilau akala na kushiba sana kitendo kilichosababisha tumbo lake kuwa kubwa ndipo akaamua kupiga picha akiwa ametunisha tumbo na kutupia mtandaoni ambapo watu walianza kumpongeza kwa kuwa na ujauzito jambo ambalo alilipokea na kulikubali.
“Kwa sababu watu walinianzishia hilo na mimi nikawa naitikia kwamba ni kweli ni mjamzito lakini sikuwa na mimba ingawa hata nilipoulizwa nilijibu kweli na nilimtaja mpaka baba wa mtoto wangu kwa kumuonesha mitandaoni lakini kwa sasa sitaki kumzungumzia kabisa,” alisema Ruby.

Post a Comment