GWAJIMA ALIASHA DUDE KWA MBWEMBWE KUPIGWA RISASI KWA LISSU!
ASKOFU wa
Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church (GCTC) ‘Ufufuo na Uzima’, Dk. Josephat
Gwajima ‘Mzee wa Dude’ ameomba kupewa muda ili ajiridhishe kabla ya kuwaanika
kwa majina watu wanaoitwa… “wasiojulikana…” walimpiga risasi na kumjeruhi
vibaya Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Wakili Tundu Antipas Augustino Mgwai Lissu ‘TL’ kiwa ni
moja ya kutimiza majukumu yake ya ki-askofu kwa kuwa hakuwa nchini kwa zaidi ya
siku 80, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Katika
mahubiri yake yaliyofurika umati mkubwa jana huku akichombeza kwa mbwembwe na
mikogo ya kijasiri, Gwajima ambaye siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu
mkubwa kutokana na tabia yake ya kuweka hadharani mambo mazito bila kujali cheo
na nafasi ya mtu, alikemea vibaya kitendo hicho na kuogeza kuwa waliomwaga damu
ya Lissu itawalilia na kisasi dhidi yao kiko mikononi mwa Mungu.
“Damu ya
kiumbe hai ina sauti na kilio, maandiko matakatifu yanathibitisha hilo kupitia
Biblia katika vitabu mbalimbali, nakuhakikishieni wale wote waliomwaga damu ya
Tundu Lissu ni lazima itawarudia, ni lazima tukemee maovu haya kwani nchi yetu
imejaa amani na utulivu hivyo hatuko tayari kuona watu wachache wanajaribu
kutuchafulia.
“Ndugu
zangu risasi ni kitu kibaya mno, inahitaji mtu mwenye ujasiri wa ajabu tu
kukamata bunduki na kumfyatulia binadamu mwenzako na kwa kweli tukio la Tundu
Lissu kupigwa risasi limetia doa kubwa mno na nataka niseme wazi kwamba nipeni
muda na nitabaini na kuwaweka hadharani watu hao, nitawataja maana sikuwepo
nchini hivyo naona kama nguvu na mtandao wangu vinalegalega, namuombea Tundu
Lissu arejewe na afya yake na ataopona kwa Jina la Yesu,” alisema Dk. Gwajima.
Naye kwa
upande wake, mdogo wa Tundu Lissu, Vincent Mgwai Lissu aliwatia simanzi waaumini waliohudhuria
kanisani hapo kwa kueleza namna ambavyo kaka yake alikuwa akifuatiliwa kwa muda
mrefu na waru wasiojulikana na kwamba hatimaye wametimiza matakwa ya mioyo yao,
jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kutumia nafasi hiyo
kuwashukuru waumini na Wanzania kwa ujuma kwa kuguswa na kumombea kaka yake
bila kujali tofauti za kiitakadi na vyama.
“Kaka
yangu amemwaga damu nyingi, lakini siku kadhaa nyuma kabla ya tukio la kupigwa
kwake risasi, alitueleza kama wanafamilia juu ya ufuatiliwaji aliokuwa
akifanyiwa na watu wasiojukana na kuanika ukweli huo kwa vyombo vya habario,
asantani kwa kumuombea na hakika sisi kama wanafamilia ya Lissu, tumeuona umoja
wa Watanzania,” alisema Vincent Lissu.
Mbunge wa
Ubungo (Chadema), Saed Kubenea aliwasihi Watanzania kuzidi kuungana pamoja kwa
kukemea na kulaani juu ya tukio hilo baya.
Post a Comment