Blac Chyna Achunguzwa Malezi ya Mwanaye
![]() |
| Angela Renée White ‘Blac Chyna’. |
MWANAMITINDO Angela Renée White ‘Blac Chyna’ amekuwa akifuatiliwa na kuchunguzwa kimyakimya na shirika la kulea watoto DCFS ili kujua malezi ya mtoto wake, Dream Kardashian kama yupo salama.
Katika sakata hilo ambalo kesi yake inatarajiwa kuwepo Septemba 18, mwaka huu, Blac alifunguka na kudai kuwa yeye ni mama mwema na hata mambo yanayoonekana kuwa anayafanya kinyume na malezi ya mtoto ikiwa ni pamoja na kuvujisha picha zake za utupu alieleza kuwa ni baba wa mtoto huyo, Rob Kardashian ndio amekuwa akifanya hayo ili kuhakikisha kuwa anamharibia.

Lisa Bloom, 55 ambaye ni mshauri wa mambo ya kisheria kwa Blac Chyna amemuelezea Blac kuwa ni mama mwenye upendo kwa mtoto wake na anapenda amani kwa mzazi mwenzake pia, hata hivyo aliweka wazi kuwa hawana habari tena ya kwamba anatakiwa kuchunguzwa tena. “Sijui ni kwa nini Rob anafanya hivyo kunichafua kwani hata picha za utupu ni yeye aliziweka mitandaoni, ameeleza jinsi nilivyokuwa namsaliti na wanaume mbalimbali hii si kweli,” alieleza Chyna.

Post a Comment