YANGA YASHIKWA SHATI NA LIPULI ZATOKA 1-1
FULL TIME
Dakika ya 94: Mchezo umemalizika kwa matokeo ya bao 1-1.
Dakika ya 93: Kwasi wa Lipuli anapewa kadi ya pili ya njano, anatoka huku akilalamika.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa kwenye benchi anaonyesha dakika 4 za nyongeza, kuna mchezaji wa Lipuli yupo chini.
Dakika ya 90: Mashabiki wa Yanga wanaonekana kukata tamaa. Mchezo bado unaendelea.
Dakika ya 88: Bado mambo magumu kwa timu zote.
Dakika ya 84: Tshishimbi anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo, analalamika lakini mwamuzi anapa kadi hiyo.
Dakika ya 79: Lipuli wanarudi nyuma, muda mwingi mpira unachezwa kwenye nusu yao.
Dakika ya 78: Yanga wanafanya mashambulizi lakini bado mambo magumu.
Dakika ya 70: Yusuph Mhilu wa Yanga anaingiam anatoka Emmanuel Martine.
Dakika ya 69: Mchezo unaendelea, wachezaji wa timu zote wanatumia nguvu kubwa kupambana.
Dakika ya 65: Tshishimbi anachezewa faulo mguuni, mchezo unasimama anatabiwa.
Dakika ya 60: Mchezo ni mgumu kwa timu zote
Dakika ya 55: Lipuli wanajibu mapigo kwa kulishambulia lango la Yanga kila wanaposhambuliwa.
Dakika ya 49: Yanga wanacheza kwa kasi lakini upinzani ni mkali.
Kipindi cha pili kimeanza.
Mapumziko
Dakika ya 47: Wachezaji wa Lipuli wanalalamika kuwa mpira ulikuwa haijaingia baada ya Ngoma kuupiga kichwa, lakini mwamuzi anaweka kati.
Dakika ya 45: GOOOOOOOOOOOOOOO!!! Yanga wanasawazisha kupitia kwa Ndoma lakini utata unatokea.
Lipuli wanapata bao kupitia kwa Seif Abdallah ambaye akicheza vizuri kwa kuwatoka walinzi wa Yanga kabla ya kufunga.
Dakika ya 44: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 42: Matokeo bado ni 0-0, timu zote hazijafanya mashambulizi makali mengi.
Dakika ya 39: Mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja.
Dakika ya 36: Kipa wa Lipuli anachezewa faulo wakati wa kona, mchezo unasimama kwa dakika mbili kisha unaendelea.
Dakika ya 33: Mchezo unaendelea kwa kasi.
Dakika ya 28: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini linakuwa halina faida.
Dakika ya 24: Lipuli wanaonyesha kujiamini na kuwabana Yanga.
Dakika ya 22: Yanga wanapata kona lakini haina faida.
Dakika ya 21: Lipuli wanaonyesha kuwa na makali, wanalishambulia lango la Yanga, almanusura wapate bao lakini mpira wa kichwa unapaa juu ya lango.
Dakika ya 18: Yanga wanaanza kupanga mashambulizi licha ya upinzani mkali kutoka kwa Lipuli inayofundishwa na Selemani Matola.
Dakika ya 11: Yanga wameshacheza faulo mara mbili, Lipuli mara 4.
Dakika ya 5: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.
Dakika ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Kipindi cha kwanza kimeanza, huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu zote zimeingia uwanjani kucheza mchezo wao wa kwanza msimu wa 2017/18.
Post a Comment