MAOMBI YA MASANJA YAJIBU! MKE WAKE SASA NI MJAMZITO
Masanja akiwa na mke wake
ANAJIBU maombi! Wakati ndoa yake ikitimiza mwaka mmoja mwezi huu
tangu ilipofungwa Agosti, mwaka jana ndani ya Kanisa la Mito ya Baraka
lililopo Jangwani jijini Dar, aliyekuwa memba wa Kundi la Vichekesho la
Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ huku masimango
yakiwa mengi kutokana na kukaa muda mrefu bila mkewe, Monica kushika
ujauzito, hatimaye Mungu amejibu maombi, Ijumaa Wikienda linakuwa la
kwanza kukupa habari njema.Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kililitonya Ijumaa Wikienda kuwa, katika ndoa ya Masanja kulikuwa na changamoto kubwa kwani chokochoko na masimango vilikuwa vimeanza huku watu wakijiuliza kwa nini miezi yote hiyo mkewe hajapata ujauzito kwa sababu watu walishazoea mtu akiingia tu kwenye ndoa muda mfupi baadaye lazima ijibu.
“Kiukweli Masanja na Monica wamepitia kwenye masimango makubwa sana kwani watu walikuwa wakiwasimanga kwamba ndoa yao imechelewa sana kujibu huku wengine wakidai huenda kuna mkono wa mtu ndiyo maana wamekawia kiasi hicho.
Masanja akiingia kwenye gari
“Masanja alikuwa akiwasilikiliza tu na kuwaacha huku akiamini kwamba siku moja watajaliwa kwani mipango yao ilikuwa siyo kupata mtoto kwa kipindi hichohicho walichofunga ndoa pia mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. “Yaani hivi sasa mke wa Masanja ni mjamzito jambo ambalo limempagawisha Masanja ambaye pia ni mchungaji huku mahaba yakizidi zaidi kwa mkewe huyo kutokana na furaha,” kilidai chanzo hicho.
AFANYA MAOMBI MAALUM
Chanzo kiliendelea kunyetisha kuwa, kutokana na masimango kuzidi, Masanja na Monica waliamua kufanya maombi maalum ya kufunga huku wakiwashirikisha wapendwa wenzao wawaombee na ndipo Mungu akajibu na mwanamama huyo sasa hachezi mbali na ndimu. “Yalifanyika maombi maalum kwa ajili ya suala la kupata mtoto ambapo walifunga kwa siku kadhaa na kweli Mungu ndiyo hivi amejibu maombi yao,” kilisema chanzo.AMFANYIA SAPRAIZI MKEWE
Hata hivyo, chanzo kiliendelea kutoa ubuyu kuwa kutokana na furaha ya kuwa baba kijacho, Masanja alimfanyia sapraizi mkewe kwa kumnunulia gari mpya aina ya Toyota RAV4 ikiwa ni shukrani kwake kutokana na suala hilo la kipekee kwake baada ya kusimangwa.MASANJA ASAKWA
Ijumaa Wikienda, baada ya kupata habari hizo, lilimtafuta Masanja kwa njia ya simu mara kadhaa wiki iliyopita, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa. Hata alipotumiwa meseji na kuelezwa juu ya ubuyu huo hakujibu hivyo jitihada zinaendelea. Hivi karibuni kwenye mitandao yake ya kijamii, Masanja alitupia picha akiwa na Monica aliyevalia vazi la mjamzito huku akiwa amemficha tumbo lisionekane.STORI: GLADNESS MALLYA| DAR ES SALAAM
Post a Comment