ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 14


“Mmh! Usiniambie.”
“Dada Shuku anayajua mapenzi anajua apige wapi kumsambalatisha mwanamke.”
“Wacha weee!”
“Nilipanga kumpagawisha lakini nimepagawa mimi.”
“Jamani mdogo wangu natamani nami nirudi umri wako nikutane wa wanaume kama Shuku.”
“We ulie umekula kwako endelea na shemeji.”
“Lakini hata shemeji yako anajitajidi akinishika mwenyewe naipata.”
“Dada mi nimeamua kuachana na MJ bora mapenzi yangu yote niliyarudishe kwa Shuku.”
“Ni kweli uamuzi wako ni mzuri, nina imani MJ humuelewi lakini ikimjua hawezi kukusumbua.”
“Dada nina moyo gani wa kuniacha hotelini mara mbili niendelee kuwa naye?”
“Sikiliza mdogo wangu mjini jua kula na kipofu, MJ mchukulie kama sehemu ya kukuingizia fedha ila penzi unalipata kwa Shuku.”
“Sawa dada lakini lazima nami nimkomeshe.”
“Mdogo wangu mwanaume hakomolewi kwa vile tupo wanawake wengi.”
“Kama angejua hilo kwa nini amenifuata akijua mimi ni mpenzi wa ndugu yake. Ukiona ona hivyo kipo kilichomvutia kwangu na kuamua kunifuata.”
“Mmh!”
“Dada usigune yaani anayonifanyie MJ si ya kumtetea.”
Wakiwa katikati ya mazungumzo simu iliingia alipoangalia alikuta ni MJ. Aliiangalia bila kuipokea kitu kilichomfanya dada yake amuulize.
“Vipi MJ nini?”
“Umejuaje?”
“Pokea.”
“Ataniambia nini?”
“Msikilize mdogo wangu, mpaka mtu anapiga ana la kusema.”
“Siwezi kumsikiliza kwa leo labda kesho sitaki kusikia sauti yake wala kuiona sura yake.”
“Haya, lakini usitumie hasira, heri Shuku angekuwa anatoa fedha ulikuwa na haki ya kuachana naye.”
“Tena nimekumbuka narudi huko huko,” Lily alisema huku akinyanyuka.
“Kuna nini?” dada yake alishtuka.
“Nikirudi nitakupa jibu.”
Lily alikwenda kuoga na kubadili nguo kisha aliingia kwenye gari na kurudi kwa Shuku akiwa na lake moyoni mwake.
Nguo alivaa nguo za usiku ziluacha mwili wake sehemu kubwa nje zilikuwa za kuvaa usiku lakini alivaa mchana kwa vile alikuwa anaendesha gari. Moyoni aliapa kumtesa MJ kama akimkuta naye aumie kwa kumuona si mali kitu kumtelekeza hotelini mara mbili.
Alipaki gari kwenye maegesho na kuingia ndani, sebuleni aliwakuta MJ na swahiba wake Shuku wakipiga stori aliwasabahi kwa furaha ya uongo kwani moyoni alimchukua sana MJ.
“Habari zenu?” aliwasalimia huku akienda kumkalia mapajani Shuku.
“Nzuri, vipi bebi mbona ghafla?”
“Kuna ubaya mtu kuja kwa mpenzi akijisikia?”
“Hakuna ubaya je, usingenikuta?”
“Ningekupigia simu, usingerudi?”
“Ningerudi.”
“Lakini nilijua usingetoka leo shughuli ya jana tuliyopeana haikuwa ya kitoto,” Lily alianza kumchokonoa MJ.
“Mmh! Jana ulikuwa kama umeahidiwa kombe.”
“Nilikuwa na usongo kuna mtu aliniudhi hasira zote nikamalizia kwako, ” alifikisha ujumbe kwa MJ bila Shuku kujua.
“Mmh! Bebi unatisha machejo ya jana mmh! Temea chini.”
“Hata uliyonipa wewe sijawahi kuona toka nilipomjua mwanaume. Kwa nini ulinibania siku za nyuma mpenzi, yaani raha za kuamkia leo zimenifanya nishindwe kukaa nyumbani na kujikuta nikikufuata unipe tena,” Lily alisema akipeleka mdomo kwa Shuku huku mkono akiteremka kwenye shamba la miwa.
Mdomo aliupokea lakini mkono ulipoanza kupekecha kama karanga Shuku alishtuka.
“Aah! Dear?”
“Nini?”
“Unataka kufanya nini?”
“Kipi cha ajabu?” Lily alihoji kwa ukali.
“Si unamuona shemeji yako?”
“Kwani hayajui haya?”
“Lakini lazima tumpe heshima yake.”
“Kipi cha ajabu hebu acha kuniudhi na mkono wangu ukiutoa tutakosana,” Lily alikuwa mkali.
“La..lakini.”
“Lakini nini? Humu ndani hiki tunachokifanya kina ugeni gani, shemu hajui sisi ni wapenzi?”
“Anajua, lakini mambo yetu tunafanyia ndani, yeye siku ile alifanyia wapi?”
Kauli ile ilimfanya Shuku awe mpole kwa vile mambo kama yale MJ siku nyingine huyafanya na wanawake zake mafyatu. Baada ya kutulia Lily aliendeleza uchokozi kwa kuteremsha bukta ya Shuku ili aanze kuchana mistari palepale sebuleni, Shuku alimsukuma na kusimama.
“Aah! Bebi unataka kufanya nini?” Shuku alikuwa mkali.
“Shuku rudi..nakwambia rudi,” Lily alinyanyuka kumrudisha Shuku wakati huo gauni lake fupi lilikuwa limepanda na kuziacha sehemu za chini tupu huku mzigo uliokuwa wazi ukiimeza bikini yote na kuonekana kama hakuvaa kitu.
“Noo, bebi twende chumbani.”
“Kwani hapa kuna nini?” Lily alizidi kuwa mkali.
“Imeanza lini?” Shuku naye alimbadilikia Lily baada kuona anakoelekea kubaya.
“Leo.”
“Sikiliza Lily mi si muhuni jiheshimu sipendi upumbavu, kukuchekea isiwe sababu nitakupiga chini na hakuna kitu chochote kitakacho pungua kwangu.”
“Basi hunipendi.”
“Kwa mtindo huu tutachokana mapema.”
“Mbona huwa wote mnaangalia mkanda wa picha chafu.”
“Kwa hiyo unashindana na mimi?”
“Hapana mpenzi wangu.”
“Na haya ndiyo mavazi gani, nilikueleza nini?” Shuku alizidi kumgeuzia kibao Lily.
“Samahani mpenzi wangu, nilikuwa ndani ya gari pia nilijua shemeji hayupo.”
“Lily jiheshimu, kama unataka kuendelea kuwa na mimi jiheshimu la sivyo tutaachana huku tunapendana.”
“Nisamehe mpenzi wangu.”
“Haya nenda chumbani mara moja,” Shuku alisema kwa sauti ya amri iliyomfanya Lily akimbilie chumbani moyoni akiamini salamu japo kidogo lakini zimefika.
Baada ya Lily kwenda chumbani Shuku alimgeukia rafiki yake na kumwambia.
“Sorry best.”
“Kawaida.”
“Hapana best sikutegemea huyu demu kuchetuka hivi.”
“Labda amekunywa, mbona ya kawaida unakuwa mgeni kwangu?”
“Lakini sikupenda tabia ile.”
“Bebi nini mwenzio hali mbaya,” Lily alitoka chumbani akiwa amejifunga taulo dodo zikiwa nje zikiwa zimejaa sawa bin sawia kifuani na kumfanya MJ kuingia kwenye mateso baada ya kujua rafiki yake anakwenda kufaidi utamu pia aliujua vizuri uwezo wa Lily anapoamua kumkata kiu mwanaume.
“Shuku kampe haki yake shemeji,” MJ alimwambia Shuku.
Lily alipokutanisha macho na MJ alimzomea kisha alimshika mkono Shuku kurudi nyumbani. Baada ya kuingia chumbani MJ alipata hamu ya kupiga chabo kutokana na mzuka alioonesha Lily alijua patachimbika bila jembe.
MJ alitulia kwa muda akiamini baada ya muda shughuli pevu itaanza, kuchelewa kwake alitaka akute watu wapo katikati ya shughuli. Baada ya kuridhika na muda aliweka alitoka nje na kuzunguka nyuma ya nyumba taratibu hadi kwenye dirisha la Shuku na kuchukulia kwa chati.
Aliweka kuwaona vizuri kwa vile pazia lilikuwa limeachia upande mmoja. Lily ambaye alikuwa ameamua kurudisha penzi lake kwa Shuku kwa nguvu zote aliamua kujitoa kwa nguvu zote kuhakikisha penzi lake linamchanganya Shuku kama kweli yeye ndiye mwenye mali basi apewa kama aliyopewa na MJ na ndoa juu.
Akiwa amefumba macho akilalamika kama mtoto wa panya baada ya raha kugonga kila kona ya mwili. Alifumbua macho taratibu ili kumuona anayempa raha zile. Hakuamini kumuona MJ kwa nje akipaga chabo alitulia kupata uhakika na kuamini ni yeye.
Kwa vile macho ya MJ yalikuwa kwenye nyasi zilizokuwa zikiumizwa na ugomvi wa tembo wawili hakuweza kumuona Lily akitazama. Moyoni alifurahi na kuamini ile ndiyo nafasi ya pekee ya kumshikisha adabu MJ baada ya kukosa sebuleni pale alikuwa amejipeleka mwenyewe.
Kwa vile dirisha lilikuwa la vioo Lily aliamini kabisa MJ anaona picha bila sauti. Alisitisha zoezi na kumwambia Shuku:
“Samahani mpenzi zima AC washa feni ya juu pia fungua na madirisha.”
“Kwa nini mpenzi?”
“Fanya kwanza kipi cha ajabu.”
Shuku akinyanyuka na kuzima AC kisha aliwasha feni ya juu na kufungua madirisha ya vioo na kurudi kitandani. MJ kidogo avunje mguu baada ya kumuona Shuku akielekea dirishani wasiwasi wake labda wamemuona.
Lakini hali ilikuwa kawaida, alitulia kusikiliza na kurudi taratibu kwa kutembelea magoti mpaka chini ya dirisha kusikiliza. Ajabu ndani alisikia ya Lily akionekana ameshikika vilivyo. Sauti ile ilimfanya MJ kujua hawakumuona labda AC haifanyi kazi.
Alirudi taratibu na kujikuta akiuona mpambano live tofauti na mwanzo aliona picha bila sauti. Hakuamini jinsi Lily alivyokuwa akitoa kilio cha mahanjamu na kumfanya uwe kwenye hali mbaya sana.
Kama kawaida Lily alijifanya yupo bize lakini jicho lake lilikuwa dirishani. Kutokana na kuchanganyikiwa MJ alikisogeza kichwa ili aone vizuri, aliweza kumuona MJ akipiga chabo hapo ndipo alifanya alichokipanga kukifanya ndipo alipopandwa wazimu wa mapenzi.
Mambo aliyoyafanya kwa ajili ya kukomoa MJ baada ya kumkosa sebuleni hukuwepo ila shetani wako alikuwepo. Mtoto wa kike alijua kujituma na kujiachia huku akilia kama mbwa aliyemuona chatu.
“Shuku unajua kuliko wanaume wote.. unajua..unajua..hapo sasa kichwa cha dhahabu.”
Mtoto baada ya kusema vile aliiachia nyonga izungumze na kumgeuza Shuku tela kumfuata anavyotaka. MJ alikuwa akikanyaga yai la pili huku akijisugua kichwa kwenye ukuta bila kujijua.
Hali ilikuwa mbaya sana kwa shuku wakati ndani shughuli ikiendelea na kilio cha Lily cha mateso kilimmaliza MJ na kujikuta akikaa chini bila kupenda baada ya kuvunja yai la tatu mkononi.
Lily baada ya kuridhika na mateso aliyompatia MJ kama kisasi cha kumdharau alimaliza mchezo akiwa hoi baada kutumia nguvu nyingi kumkomoa MJ. Naye Shuku alikuwa hoi baada na yeye kwenda marikiti zaidi ya mara tatu.
Walijilaza na usingizi uliwapitia kila mmoja alilala kama wahanga wa ajali ya meli.
Nje MJ baada ya kupata nguvu na wakati huo ndani palikuwa kimya alinyanyuka na kuchungulia na kuwakuta wamepitiwa usingizi kila mmoja amelala mlalo wa hasara.
Alirudi nndani huku akijipanga katika siku zile mbili lazima awe na Lily ili naye apate penzi kama lile huku akiapa kumnunulia gari la bei mbaya. Baada ya kuoga alilala kwani naye alikuwa amechoka kwa kusafiri kwenye bahari ya nchi kavu. Alipanda kitandani na usingizi ulimchukua.
*****
Lily baada ya kutimiza alilolitaka, baada ya kuamka alikaa sebuleni na kumwacha Shuku amejilaza ili amsikie MJ anasemaje. Akiwa anaangalia muvi alimuona MJ akisogea kwenye kochi alilokuwa amekaa.
“Lily,” alimwita kwa sauti ya chini ili Shuku asisikie.
“Jina langu,” Lily alimwitikia huku akiangalia pembeni umebinua midomo.
“Mbona mkali mpenzi.”
“Mpenzi wako nani?”
“Najua nimekuudhi jana usiku nilipata dharula nakuahidi kukulipa fidia yoyote utakayo.”
“Uliyonifanyia nashukuru, asante sana unatumia fedha zako kunidhalilisha, asante mwili wangu si umeutumia inatosha itabakia stori. Unatendelea kubakia shemeji yangu hilo halitabadilika lakini mapenzi na mimi sahau.”
“Usifanye hi...” MJ alikata kauli baada ya kusikia nyayo za miguu ya Shuku kuja sebuleni.
“Vipi best nipo na shemeji langu la nguvu,” MJ alijibalaguza.
“Hakuna tatizo, nilipitiwa na usingizi kidogo.”
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA

KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
SEHEMU YA 9==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-09.html
SEHEMU YA 10 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-10.html
SEHEMU YA 11 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-11.html
SEHEMU YA 12 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-12.html
SEHEMU YA 13 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-13.html

:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.

Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.
a kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

No comments

Powered by Blogger.