KIUNGO YANGA TSHISHIMBI APEWA GARI LA SH MIL 100
BAADA ya kelele za kumsifu kuwa nyingi, Yanga imempa kiungo wake Papy Kabamba Tshishimbi gari la kutumia lenye thamani ya Sh milioni 100. Tshishimbi anasifiwa kwa kufanya vizuri katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Jumatano wiki hii.
Fasta baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga ikafungwa kwa penalti 5-4, kiungo huyo alikabidhiwa gari likiwa na dereva wake kwa matumizi binafsi. Yanga imeamua kumpa Tshishimbi raia wa DR Congo gari hilo aina ya Ford Ranger lililo katika muundo wa ‘Double Cabin’ lenye rangi ya chungwa na jana alionekana nalo mazoezini Uwanja wa Uhuru.
Papy Kabamba Tshishimbi akiingia katika gari alilopewa aina ya Ford Ranger lililo katika muundo wa ‘Double Cabin’ .
Gari analotumia Tshishimbi kama ukilitaka jipya lake utalazimika kutoa si chini ya Sh milioni 100, kwa kuwa ndiyo bei yake kwani mengi yake ni mapya na yanatoka kiwandani Afrika Kusini. Tshishimbi amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland na baada ya kucheza mechi mbili tu, amejizolea umaarufu mkubwa nchini.
Ford Ranger lililo katika muundo wa ‘Double Cabin’.
Championi Jumamosi jana asubuhi lilimshuhudia Tshishimbi akiwasili katika mazoezi ya Yanga akiwa ndani ya gari hilo akiendeshwa na dereva maalum na baada ya mazoezi hayo aliondoka naye. Bosi mmoja wa Yanga akigoma kutajwa jina lake, alisema: “Tumempa gari Tshishimbi kwa matumizi yake ya kawaida kama kwenda mazoezini na kurudi, hili ni jambo la kawaida kwetu.
“Huyu kiungo anakaa Mbezi sasa bila gari anaweza kupata tabu ya kuwahi mazoezini ukizingatia ni mgeni hapa nchini, gari hili atalitumia katika muda huu na yeye analitumia tu.” Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema: “Hilo gari Tshishimbi analitumia tu kwa kuwahi na kutoka mazoezini kwenda kwake, haimaanishi kama klabu imempa moja kwa moja.”
Akiendelea kukagua garui lake hilo.
Ten alisisitiza kuwa, Tshishimbi atalitumia gari hilo kwa matumizi ya kawaida na isieleweke kwamba amepewa ‘mazima’. Mbali na Tshishimbi ambaye analitumia gari hilo, Amissi Tambwe yeye ana gari binafsi Toyota Land Cruiser pia Ibrahim Ajibu anamiliki gari aina ya Toyota Brevis alilolipata baada ya kusajiliwa na Yanga akitokea Simba.
HABARI NA CHAMPIONI
Post a Comment