Viongozi Wamiminika Nyumbani Kwa Marehemu Ndesamburo Kutoa Pole Kwa Familia
Maandalizi ya mazishi ya marehemu Dkt, Philemon Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
akitoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu Ndesamburo, Ndehorio
Ndesamburo, alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia.
Mwenyekiti
wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe, akitoa mkono wa pole kwa mjane Ndehorio Ndesamburo
nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
...Akitoa mkono wa pole kwa Filomena Ndesamburo, mtoto wa Ndesamburo nyumbani kwao.
Waziri wa Malisili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mjane wa marehemu Ndesamburo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma, akitia saini
katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John
Mrema, akitia saini katika kitabu cha waombolezaji.
Baadhi ya madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji .
Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Ndesamburo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu, Saidi Meck Sadiki (kushoto)
akisalimiana na Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu
Ndesamburo.
...Akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Ndesamburo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa tatu kulia) akisalimiana na mume wa
Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, Dkt Fidelis Owenya alipofika
nyumbani wa marehemu Ndesamburo kutoa salamu za pole.
...Akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa Ndesamburo.
Mjane wa marehemu Ndeamburo, Bi Ndehorio Ndesamburo (kulia ) akiwa mwenye huzuni.
Baadhi ya waombolezaji .
Mbowe akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu Ndesamburo .
Baadhi ya watoto wa marehemu Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
(Picha Na Dixon Busagaga -Kanda ya Kaskazini.)
Post a Comment