Roma, Snura na Stamina ‘Wamwaga’ Mafuta Kwa Bodaboda
Roma alikuwa ameambatana na wasanii wenzake wawili, Snura na Stamina, ambao watafanya shoo pamoja katika Ukumbi wa Dar Live siku ya Iddi Mosi ambapo waliongea na waandishi wa habari kuhusu jinsi watakavyotoa burudani siku hiyo.
Hafla hiyo na waandishi wa habari ilifanyika katika Uwanja wa Zakhem-Mbagala jijini Dar es Salaam.
Roma alitamba kwamba atawabeba mashabiki zake na kuwafikisha salama katika shoo hiyo.
Msanii huyo maarufu ambaye shoo hiyo itakuwa ni ya kwanza toka apatwe na janga hilo, alisema licha ya mafuta hayo, pia siku hiyo atakuwa na ‘surprise’ kibao kwa mashabiki wote watakaojitokeza ukumbini hapo, kwani shoo hiyo ni ya muhimu sana kwake.
“Naomba nianze surprise zangu kwa kuwawekea mafuta baadhi ya rafiki zangu 50 wa bodaboda, kwani hawa ndiyo nguzo kubwa kwangu siku hiyo ya Iddi Mosi.
“Wao ndiyo watakaobeba baadhi ya mashabiki zangu kuwaleta kwenye shoo na kuwarudisha makwao salama.
“Shoo hiyo itakuwa ya aina yake kwa sababu nikiwa jukwaani nitakuwa nimezungukwa na mastaa wenzangu kama Stamina, Snura ambao mnawaona hapa, lakini ukiachana na hawa kutakuwa na Darassa, pia utapata fursa ya kusikia kidogo vionjo vya mwambao kutoka kwa Zanzibar Star na Mr Blue kwa bei ya shilingi 7,000 tu.
“Naomba kutumia muda huu kuwakaribisha wale wote wapenda burudani kwani waje wakijua kwamba siku hiyo ya Iddi Mosi burudani itakuwa sehemu moja tu hapa Dar es Salaam, na mahali sahihi ni Dar Live, hapo ndiyo utakutana na wakali wa michano wenye uwezo wa kila aina,” alisema.
Post a Comment