RAYUU: ‘WOLPER APIME UKIMWI’
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye.
“Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
“Kutokana na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu yake.”
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Kutokana na mtafaruku huo, mapaparazi wetu walifanya juhudi za
kumsaka Wolper pasipo kuzaa matunda, ambapo simu yake ya kiganjani
iliita bila kupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wenye
mlolongo mzima wa ishu hiyo, hakujibu.

Post a Comment