Usiku wa June 3 2017 katika uwanja wa
Millenium jiji la
Cardiff nchini
Wales Real Madrid waliandika historia mpya katika uwanja huo baada ya kufanikiwa kutwaa taji lao la 12 la
UEFA Champions League katika historia ya club yao.
Real Madrid walitwaa taji hilo baada ya kufanikiwa kuifunga
Juventus ya
Italia kwa jumla ya magoli 4-1, baada ya ushindi huo wa
Real Madrid leo June 4 wamewasili nyumbani kwao
Hispania na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wao.
Baada ya kuwasili Hispania
Real Madrid walikaribishwa katika ukumbi wa City Hall jijini
Madrid na baadae kutoka nje kuwasalimia maelfu ya mashabiki wao waliyojitokeza kufurahia ushindi huo, sherehe za Ubingwa wa
Madrid zinaendelea usiku wa leo katika uwanja wao wa
Santiago Bernabeu.
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akimkabidhi Kombe la UEFA Rais wa jiji la Madrid Cristina Cifuentes
Mashabiki waliyokuwa wamejitokeza kwa nje
Sergio Ramos akimkabidhi jezi Cristina Cifuentes inayooneshwa wametwaa taji la UEFA kwa mara ya 12.
Cristina Cifuentes na Sergio Ramos
Cristina Cifuentes na Rais wa Club ya Real Madrid Florentino Perez
Cristina Cifuentes, Sergio Ramos na Rais wa Club ya Real Madrid Perez
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos baada ya kumkabidhi jezi Meya Manuela Carmena
Post a Comment