Mama Lulu Akwepa Mtego wa Lulu kuchumbiwa!
UCRESIA Kalugira ambaye ni mama wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameruka mtego wa mwanaye kuchumbiwa tena baada ya mmoja wa mapaparazi wetu kufika nyumbani kwake na kujifanya ni muoaji.
Paparazi huyo aliyekuwa ameongozana na mwenzake, walifika nyumbani kwa mama Lulu Jumatatu iliyopita na kukuta nyumba imepigwa kufuli ndipo walipompigia simu baada ya Lulu kutopatikana, mazungumzo yakawa hivi:
Paparazi: Tuko nyumbani kwako hapa, tuna jambo la heri.Msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mama Lulu: Nyie ni nani, ni jambo gani hilo maana sipo nyumbani.
Paparazi: Tunaishi hapa Tegeta, tuna barua tumeleta posa ili kumuoa binti yako.
Mama Lulu: Mmeleta posa!? Mmeshawasiliana na Eliza mwenyewe?
Paparazi: Hapana ila tumeona tuje kwako maana wewe ndiye mzazi unaweza kutuambia tu kama nafasi ipo.
Mama Lulu: Mtaniulizaje kama amechumbiwa au laa? Nyie kuna kitu mnatafuta! Nadhani mtafuteni Lulu mwenyewe ndiyo mje kwangu, hata hivyo sidhani kama anataka kuolewa (akakata simu.)
Chanzo: Gazeti la Amani
Post a Comment