ad

ad

G Nako na Belle 9 waona fursa kwenye harusi

Wasanii G Nako na Belle 9 katika project yao mpya ‘Ma-Ole’ ni kwa ajili ya kusherehesha kwenye harusi, na ni mwanzo wa kuwaandikia maharusi nyimbo kwa wale watakaohitaji.
G Nako na Belle 9
Belle 9 amesema wakati wanatoa wimbo ‘Give It To Me’ akiwa na G Nako walipata show kadhaa za pamoja ambazo walienda kufanya kwenye harusi tofauti tofauti ndipo wakawaza kuja na wazo jipya la kutengeneza pesa kupitia harusi.

“Ma- Ole maana yake  ni My Only kwa kingereza, kwa sababu hii tumeudedicate moja kwa moja mtaani kwa watu wa kawaida, kwa mashabiki wetu kama watakuwa na harusi. Mimi na G Nako kwa sasa hivi tunaandika stori yako na mtu wako toka mmekutana, mnatuelezea tunaandika halafu tunakuja kuperform kwenye harusi yako ,” amesema Belle 9.
By Peter Akaro

No comments

Powered by Blogger.