Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996
KIUKWELI
tarehe kama ya leo miaka 21 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi
kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia
Mei 21, 1996, meli ya MV Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800
pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa
Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi
kavu.
Ripoti
ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza
kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa
wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya
Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na
jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.
Hakika
Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo
kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu
Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama
hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.
Mkoani Kagera.
Meli
ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani
850 na abiria 430 ilizama katika Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza
yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka ufukweni mwa maji na
kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika Meli hiyo ambayo
tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo
la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa
ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba abiria 430).
Pengine
tumezoea kuita kwamba Mei 21 Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya
kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani
kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja
Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
Wakati
leo tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu
tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo imani ya watalaamu wa masuala ya
usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri (Picha zote na Maktaba).
Lakini
wakati tunatafakari suala hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe
bila kusubiri kusukumwa na mtu hususani wale wenye mamlaka ya kuleta
matokeo chanya katika kuboresha hali ya usafiri majini Ikiwemo Mamlaka
ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA kwamba tulijifunza jambo
lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?
Na
Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo
jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya
kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa
majini na nchi kavu? Je, tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za
uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu?.
Lakini
pia wapo waliohoji na bado wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti
ya uchunguzi wa ajari hiyo ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo?
Lakini pia wakiwa bado wanaendelea kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo
vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo? Hapo nadhani nawe
unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na
kuyagharimu maisha ya Watanzania ikiwemo ile ya mv Spice Ireland
iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika Mkondo wa Nungwi kaskazini
Unguja Zanzibar.
Lakini
yote Tisa, Kumi ni stofahamu iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo
mbaya kuwahi kutokea hapa nchini.Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa
Wakaguzi wa na Waangalizi kwa maana ya Mamlaka husika, Wapo waliosema
ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na Timu yake na wapo waliosema chombo
kilikuwa kibovu.
Wapo
waliodai chombo hicho kilikuwa kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo
wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe walisababisha ajali hiyo kwani
walilazimisha kupanda Melini ilihali chombo kilikuwa kimejaa huku
mlolongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali hiyo na Imani za
Kishirikina.
Mimi
nasema sina nia ya kuandika hayo yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila
lengo langu ni kuyaweka wazi hayo yote ili kila mmoja kwa namna
anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna ya kufanya ili kuepukana na
ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine husema tusiangalie tulipoanguka
bali tuangalie tulipojikwaa.
Wapo
wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao na mmoja wao ambae
alimpoteza mpendwa wake katika maisha yake ni Mwanamitindo maarufu hapa
nchini ambae pia anafanya shughuli zake barani Ulaya Flavian Matata
ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi pamoja na binamu yake.
Pamoja
na watu wengine, Matata amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa
kufika Mkoani Mwanza katika eneo la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza
maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyika kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyika kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
Hakika inauma sana.
Post a Comment