Tanzania Yang'ara viwango vya FIFA, imepanda Kwa nafasi 22
Tanzania
imepaa kwa nafasi 22 hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 kati ya
mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na
FIFA leo Aprili 6, 2017.
Hivi
karibuni, Tanzania katika mechi za kalenda ya FIFA, iliwashinda
Botswana na Burundi katika michezo miwili tofauti zilizofanyika Machi,
mwaka huu.
Katika
viwango hivyo vipya vya mwezi April, Brazil imeishusha Argentina
kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Argentina ikishuka
hadi nafasi ya pili na Ujerumani imebaki katika nafasi yake ya 3.
Katika ‘top ten’, mataifa yanayofuata ni Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania inakamata nafasi ya 10
Barani
Afrika Misri inaongoza ikiwa nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal katika
nafasi ya 30, Cameroon nafasi ya 33, Burkina Faso nafasi ya 35,
Nigeria nafasi ya 40 na Congo DR nafasi ya 41 ikiwa mbele ya Tunisia kwa
nafasi moja
Kwa
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda bado inaongoza ikiwa
imepanda kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 72, ikifuatiwa na Kenya nafasi
ya 78, Rwanda nafasi ya 117, Ethiopia nafasi ya 124, Tanzania nafasi
ya 135 na Burundi imeshuka kwa nafasi mbili hafasi ya 141.
Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 194 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206
Post a Comment