Yanga Yashinda bao 1-0 Dhidi ya Azam, Wanaongoza mbele ya Simba kwa pointi
MPIRA UMEKWISHAAAAAA....
KADI Dida analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
-SUB Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Msuva
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 89, Yanga wanaendelea kupoteza muda lakini wakipata nafasi wanazitumia vizuri lakini Aishi Manula anaonekana kuwa vizuri
Dk 74, Azam wanafanya shambulizi, Sure Boy anaachia mkwaju lakini Dida kama nyani anadaka
GOOOOOOOO Dk 70, mabeki wa Azam FC walitegeana kati ya Amoah na Mohamed, Chirwa akaiwahi pasi ya Niyonzima na kuwaaadhibu kwa mkwaju mkali uliogonga mwamba wa juu na kujaa wavuni
Dk 70 Mpira unaonekana kupunguza kasi, lakini kila upande unacheza taratibu
SUB Dk 69, Anakwenda nje Singano na Joseph Mahundi anaingia kuongeza nguvu upande wa Azam FC
Dk 68, Chirwa anaunganisha krosi ya Juma Abdul lakini mpira unaishia mikononi mwa Dida
KADI Dk 47, Sure Boy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Martin
DK 46, krosi nzuri ndani ya lango la Yanga lakini Chilunda anaukosa mpira hatua chache kutoka lango la Yanga
Dk 45, Mpira umeanza ikionekana kila timu inataka kupata bao la mapema na kumaliza mchezo
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, krosi nzuri kabisa ya Haji Mwinyi kali hakuna mtu ndani ya eneo la Azam FC
Dk 44 sasa, Yahaya anatolewa nje baada ya kukaa chini kutokana na maumivu ikiwa ni mara ya tatu kwake katika mechi hii leo. Anatolewa nje tena na machela
Dk 43 tena, Sure Boy anaachia mkwaju mkali baada ya Bossou kuboronga, lakini goal kickDk 31, krosi safi ya Gardiel, Sure Boy anaachia shuti lakini hakulenga lango
SUB Dk 30, Emmanuel Martin anaingia kuchukua nafasi ya Zulu ambaye ameumia
Dk 28, Zulu anatolewa nje akiwa kwenye machela baada ya kuumia huku akilia, inaonekana akilia kwa maumivu, lazima hataendelea
Dk 26 Zulu anaachia shuti kali kabisa hapa. Goal Kick, lakini yuko chini, atakuwa aligonga mguu wa HimidDk 23 Yanga wanajaribu kufanya shambulizi lakini hakukuwa na umakini
Dk 21, Himid Mao anamuangusha Msuva na kulambwa kadi
Dk 19 sasa, hakika Azam FC wanaonekana kutawala zaidi eneo la katikati wakifanya wanavyotaka. Yanga wanaonekana ni wapole na hakuna shambulizi kali wanalopeleka
KADI Dk 15, Bossou analambwa kadi ya njano kwa kumparamia Singano ambaye ametibiwa tayari
Dk 12, Yahaya anaachia shuti kali lakini goal kick
Dk 11, Azam FC wanagongeana vizuri na kuingia kwenye lango la Yanga lakini Makapu anaokoa hatari
Dk 9, Gardiel anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Chirwa na kuwa konaaa. Inachongwa hapa lakini hakuna kitu
Dk 8, krosi safi ya Singano, Chilunda anaruka na kupiga kichwa lakini Cannavaro anaokoa tena
Dk 6, Dida analazimika kuwahi kutoka na kuokoa mpira mikononi mwa Sure Boy
Dk 5, basi nzuri ya Msuva lakini Juma Abdul anashindwa kuuwahi
Dk 3, Cannavaro anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa, kona. Inachongwa na Singano, Yanga wanaokoa vizuri
Dk 2, Azam FC wanaonekana kugongeana vizuri katika eneo la kati ya uwanja, lakini hakuna mamdhahara kwenye lango la timu yoyote
DK 1, mechi imeanza taratibu huku kila upande ukionekana haujatulia vizuri
TAKWIMU
Kabla ya mechi hii, Yanga na Azam FC zimekutana mara 17. Mechi ya leo inakuwa mechi ya 18 tokea zilipoanza kukutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2008-09.
Dk 5, basi nzuri ya Msuva lakini Juma Abdul anashindwa kuuwahi
Dk 3, Cannavaro anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa, kona. Inachongwa na Singano, Yanga wanaokoa vizuri
Dk 2, Azam FC wanaonekana kugongeana vizuri katika eneo la kati ya uwanja, lakini hakuna mamdhahara kwenye lango la timu yoyote
DK 1, mechi imeanza taratibu huku kila upande ukionekana haujatulia vizuri
TAKWIMU
Kabla ya mechi hii, Yanga na Azam FC zimekutana mara 17. Mechi ya leo inakuwa mechi ya 18 tokea zilipoanza kukutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2008-09.
Kati ya hizo, rekodi zinaonyesha hivi;
Yanga IMESHINDA 5
Azam FC IMESHINDA 5
SARE 7
Post a Comment