Kairuki: Serikali Haitamvumilia Mtumishi Mwenye Cheti Feki
Inakadiliwa
kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu
na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya
kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.
Hayo
yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa
Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo,
ambapo amesema kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na
changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.
Aidha
Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye
atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua
madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku
akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao
wanataka kupora ajira za wenzao.
Post a Comment