ad

ad

Breaking News: Basi la Borussia Dortmund Lapigwa na Milipuko, Mechi Yao na Monaco Yaahirishwa



MILIPUKO mitatu imelipiga basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya Borussia Dortmund kuelekea katika mechi yao ya nyumbani ya Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya dhidi ya Monaco usiku huu.
Katika milipuko hiyo, beki wa timu hiyo, Marc Bartra (pichani juu) amejeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Mechi yao dhidi ya Monaco iliyokuwa ipigwe leo saa 3:45 usiku imeahirishwa hadi kesho saa 7:45 usiku.

Taarifa kutoka klabuni hapo imeeleza kuwa wachezaji wengine wapo salama na hakuna hatari zaidi ndani au nje ya uwanja.

No comments

Powered by Blogger.