YouTube Kuja Na Huduma Ya Kulipia Bundle La TV
Mtandao ndio kila kitu siku hizi, kila linapotokea jambo huwa ni rahsi sana kulijua ama kuliona moja kwa moja kupitia mtandao, iwe live au recorded ushindani wa mtandao umekuwa mkubwa sana na ndio maana YouTube wameamua kujiongeza na kukusogezea hii mpya.
Kizazi cha mtandao kinazidi kuwa kikubwa licha ya kuwa bado kuna mamilioni ya watu duniani ambao bado wanapenda kutazama TV za kawaida (Traditional TV), mwenendo wa kibiashara hauwezi kulifumbia jicho kizazi hiki cha kidigitali na ndio maana YouTube imejipanga kuisogeza kwetu huduma ya Streaming TV kwenye viganja vya mikono yetu.
YouTube Streaming TV ni huduma itakayowalenga wale watu (The YouTube Generation) wanaopenda kuangalia kile wakitakacho, muda wowote wautakao, kwa njia yoyote waitakayo na mahali popote watakapo. Kwa mujibu wa blog yao, YouTube imetoa listi ya aina tofauti za chanels za ku-subscribe kwa kiasi cha bundle la $35 kwa mwezi ambayo ni sawa na shillingi 78,200/= za Kitanzania.
(Imetafsiriwa hapa chini)..
” Huduma
ya YouTube TV itakuwezesha kulipia bundle ambalo litakuwa ni nusu ya
kile unacholipia kupata huduma ya chanel zako pendwa kwenye kingamuzi
cha kawaida, na wala haikulazimisha kuilipia kila mwezi. Malipo ya
kujiunga na huduma hii ni $35 (Tzs.78,200) na unaweza kujiondoa kwenye
huduma hii muda wowote“. – YouTube.

Post a Comment