TAIFA STARS WAITUMBUA BURUNDI YA KINA MAVUGO, MSUVA, MBARAKA WAKING'ARA
Taifa
Stars imeendeleza ushindi baada ya kuitwanga Burundi katika mechi ya
kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inashinda mechi ya pili mfululizo baada ya kuitwanga Botswana kwa mabao 2-0, Jumamosi iliyopita.
Huku
ikicheza bila nahodha wake, Mbwana Samatta ambaye amerejea mapema
Ubelgiji kujiandaa na michuano ya Europa League, ilionyesha kiwango
kizuri.
Ushindi wa leo haukuwa rahisi kutokana na umahiri wa wachezaji wa Burundi wakiongozwa na Laudit Mavugo.
Stars
liana kupata bao lake la kwanza kupitia Simon Msuva ambaye aliunganisha
krosi ya Mohamed Zimbwe iliyotua kichwani mwa Ibrahim Ajibu kabla ya
kumfikia mchungaji.
Mavugo aliisawazishia Burundi akimhadaa Deogratius Munishi aliyetoka langoni mapema.
Lakini
Mbaraka Yusuf anayetokea Kagera Sugar, ikiwa ndiyo anaanza kuichezea
Stars, akafunga bao zuri kabisa baada ya mpira wake wa kwanza kugonga
mwamba, lakini akamalizia kwa shuti la mguu wa kushoto.
Juhudi za Burundi kukomboa au Taifa Stars kuongeza, hazikuzaa matunda hadi mwisho wa dakika 90.
Post a Comment