Vigogo wa IPTL (Rugemarila na Seth) Wapandishwa Mahakamani Tena na Kuongezewa Mashitaka
Mfanyabiashara
Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira wamepandishwa kizimbani kwa
mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na
mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.
Miongoni
mwa mashtaka hayo 12 ya uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya
kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh
309,461,300,158. 27.
Akiwasomea
hati mpya ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro
kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alidai wanakabiliwa na mashtaka ya
kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kighushi, kutoa nyaraka za
kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia
Serikali hasara na kutakatisha fedha.
Washtakiwa
hao katika shtaka la kwanza wanadaiwa, Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi
wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, Sethi ambaye ni Mwenyekiti
Mtendaji wa PAP wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19,
2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini,
Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kimaro
alidai katika shtaka la pili la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao
kati ya Oktoba 18, 2011na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam wakiwa
siyo watumishi wa umma na watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa
uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Kwa
upande shtaka la tatu, Sethi anadaiwa kuwa Oktoba 10, 2011 katika
mtaa wa Ohio Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu
namba 14 ya usajili wa makampuni na kuonyesha yeye ni mtanzania
anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.
Seth
katika shtaka la nne anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu
namba 14a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajili wa kampuni, Seka
Kasera kwa njia ya kuonyesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa
wa Mrikau.
Katika
shtaka la tano, washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29,
2011 na Januari 23, 2014 makao makuu Benki ya Stanbic Kinondoni na
Benki ya Mkombozi Tawi St Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia
kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Sh
309, 461,300,158.27.
Katika
shtaka sita la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa
Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa
vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na
Sh 309,461,300,158.27.
Kimaro
alidai katika la saba, kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 23,
2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la
kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT USD 22,198,544.60 na Tsh
309,461,300, 158.27 wakati wakijua fedha hizo zao la kujihusisha na
genge la uhalifu.
Shtaka
la nane, Kimaro alidai kuwa Novemba 29, 2013 katika tawi la kati la
Benji ya Stanbic Tanzania Wilaya ya Kinondoni Sethi alitakatisha fedha
kwa kuchukua BoT USD 22,198,544.60 wakati akijua fedha hizo zimetokana
na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Kwa
upande wa shtaka la tisa, Sethi anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013
na Machi 14,2014 katika tawi la kati la Benji ya Stanbic Kinondoni Dar
es Salaam alitakatisha fedha, Sh 309,461,300,158.27 kutoka BoT wakati
akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Shtaka
ya kumi, inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St
Joseph Cathedral, Rugemalila alitakatisha fedha, Sh 73, 573, 500,000
kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la
kujihusisha na genge la uhalifu.
Kwa
upande wa shtaka la 11, Kimaro alidai kuwa Januari 23,2014 katika Benki
ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha
USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la
uhalifu.
Shtaka
la 12, Seth anadaiwa kuwa Januari 28, 2014 katika tawi la kati la Benki
ya Stanbic Wilaya ya Kinondoni alihamisha Rand (zar 1,305,800 kwenda
kwenye akaunti namba 022655123 katika Standard bank Land Rover Sandton
Johannesburg wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo
zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.
Washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hao.
Upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai 14, 2017.
Hata hivyo mashtaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana.
Post a Comment