ad

ad

Siwema: Nay Anakurupukaga, Nilitarajia serikali kumpa kashikashi kutokana na wimbo wake wa Wapo



MZAZI mwenziye na Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,  Siwema Hudson amesema kitendo cha serikali kumpa kashikashi kutokana na wimbo wake wa Wapo hakikumshangaza kwani alitarajia hayo yatokee kwa kuwa zilipendwa wake huyo ni mtu wa kukurupuka.

Akizungumza  juzi baada ya Nay kutoka polisi, Siwema alisema yeye amekaa na Nay kwa muda mrefu na mara nyingi akiamua jambo ndiyo hivyo wala hakuna mtu anayeweza kumshauri.

“Unajua Nay anapenda kukurupuka na wala hataki mtu apinge wazo lake, kama ameamua kufanya kitu anafanya tu na nilifahamu kuwa ipo siku hilo lingemtokea, sasa kama limepita anatakiwa kujitathmini upya,” alisema Siwema


CREDIT: GPL

No comments

Powered by Blogger.