Bajeti ya Kenya ya mwaka 2017/2018 Yasomwa.....Ajira Sekta ya Umma Zasimamishwa
Bajeti
ya Kenya ya mwaka 2017/2018, imesomwa jana kinyume na inavyosomwa
kawaida mwezi Juni, kutokana na uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka
huu, huku ikitangaza kusimamisha ajira katika sekta ya umma.
Katika
bajeti hiyo ya shilingi za Kenya trilioni 2.6 (Takriban shilingi
trilioni 52 za Tanzania) Waziri wa Fedha, wa nchi hiyo, Henry Rotich
ameondoa kodi kwenye mahindi yanayoagizwa kutoka nje kwa kipindi cha
miezi minne ijayo,
Aidha kodi imeondolewa kwenye dawa za kuulia wadudu za nchini humo pamoja na magari ya utalii yanayoundwa nchini Kenya.
Katika
bajeti hiyo ambayo ni ya mwisho kwa serikali ya Jubilee katika muhula
wake wa kwanza, serikali imeongeza kodi kwenye kamari hadi 50% kutoka
7.5% ya awali kama njia ya kukomesha uchezaji kamari.
Serikali pia imetangaza kusimamisha ajira katika sekta za umma isipokuwa sekta ya elimu kama njia ya kupunguza matumizi.
Jumla ya Shilingi bilioni 524.6 za kenya katika bajeti hiyo zitatokana na mikopo kutoka nje na ndani ya nchi.
Shilingi
bilioni 2 za Kenya zimetengwa kuwaajiri walimu, na zingine bilioni 4
kuwalipia mtihani wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nnemwaka
2017 na 2018 huku serikali za kaunti zikipata jumla la shilingi bilioni
329.
Ili
kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi milioni
450 Ksh kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni 250
kuboresha kiwanda cha maziwa cha New KCC.
Post a Comment