Neema Wambura Amshukuru Rais Magufuli Kwa Kumsaidia, Awapongeza Madaktari na Wauguzi
Mgonjwa
Neema Wambura ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) amemshukuru Rais John Pombe Magufuli baada ya afya
yake kuimarika na kuruhusiwa leo kurejea nyumbani.
Neema amemshukuru rais kwa kumwezesha kupata matibabu tangu alipofikishwa katika hospitali hiyo Februari 23, mwaka huu.
“Namuomba
Mwenyezi Mungu amuepushe Rais Magufuli na mambo mabaya yote. Sasa
nipata nguvu, nina furaha na naoga mwenyewe tofauti na awali,” amesema
Neema.
Pia, Neema amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia huduma bora na kumwezesha kupona majeraha ya moto.
Neema
ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Mara alimwagiwa maji ya moto na mumewe
wakati alipokuwa akichemsha maji kwa ajili ya kupika ugali na kuungua
sehemu ya kifuani, shingo na mkono.
Mkuu
wa Idara ya Upasuaji na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk Ibrahim Mkoma
amesema afya ya Neema inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji
sehemu ya shingoni ili kutenganisha shingo na sehemu ya kifua na kuziba
majera ya moto.
“Neema
anaendelea vizuri sasa anaweza kunyanyua shingo vizuri kabla ya hapo
alikuwa hawezi kuinyanyua wala kuizungusha,” amesema.
Post a Comment