ad

ad

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Atoa Msaada wa Chakula Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema


Kutoka Sengerema - Mwanza.
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Kaseko  tarehe 27 Machi, 2017 ametembelea Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema na kutoa Msaada wa Chakula kwa Wagonjwa wenye hali ngumu ya Maisha & Wanaohitaji msaada kutoka kwa wasamalia wema.

Akikabidhi msaada  huo kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo  Sr. Mariojose kwa niaba ya Wagonjwa wamama na watoto Ndugu Kaseko ametoa Chakula Mahindi Kilo 100, Maharage Kilo 50, Soya Kilo 50, Sukari Kilo 25, Mafuta ya Kupikia Ndoo moja ya lita 20, Sabuni & Juice Vyenye thamani ya Tsh. 700,000/=

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha amesema yeye ni mzawa wa Sengerema na amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo wakati wote wa utoto wake hivyo anazifahamu sawia changamoto zinazoikabili huduma ya afya hospitalini hapo na kwamba ameguswa sana Matatizo hayo hivyo na kuamua kuunga Mkono Juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania katika sekta ya Afya.

Ndugu Kaseko ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbaliwa maendeleo kuisaidia Serikali kuwaletea maendeleo wananchi kwani Serikali ina mambo mengi hivyo peke yake haiwezi ni lazima watu wenye moyo wa kujitolea na wanaopenda maendeleo wajitoe kuisaidia Serikali inaayoongozwa na Rais Magufuli ambayo ukweli inajikita haswaa kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo teule ya Wilayaya Sengerema Sr.Mariojose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo na kusema ni wachache sana wenye moyo huo na kumuomba aendelee na moyo huo huo wa kujitolea wa kuwasaidia wenye Shida hasa Masikini.

Katika hatua nyingine Ndugu Kaseko amekabidhi Madawati Kumi na Tano  manne  ( 4 ) Katika Shule ya Msingi Ibondo Wilayani Sengerema. Ndugu Kaseko ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha amesema anaunga mkono Juhudi za Serikali ya Hawamu ya Tano Chini ya Rais Magufuli na Kwamba Elimu bure imekuja na changamoto kedekede kote nchini na kwamba  serikali inastahili kusaidiwa ili kuhakikisha Elimu bora inatolewa. Ndugu Kaseko ametaja baadhi ya Changamoto hizo ni Uchache wa  Madarasa ya kusomea, Maabara, Madawati, Vyoo vichache ikilinganishwa na Idadi kubwa ya Wanafunzi walioandikishwa.

Ndugu Kaseko amewaomba wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kuunga Mkono Sera ya Elimu Bure kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa kujitoa kusaidia jamiI zinazotuzunguka.

Baada ya Makabidhiano hayo Afisa Elimu Kata hiyo ya Ibondo Ndugu Janerose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo wa Madawati, Madirisha na Katoni mbili za Madaftari.

Na kwa upande Mwingine Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Emmanuel Mashili amemshukuru Diwani wa Kata hiyo Mh. Mathias Henyenge ambaye pia ni rafiki wa Ndg. Kaseko kwa Juhudi zake kubwa za kuwatumikia wananchi wa Kata ya Ibondo. 

No comments

Powered by Blogger.