Fedha za maendeleo zaongezeka kwa asilimia 36
Katika bajeti hiyo, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka trilioni 11.8 mwaka 2016/17 hadi trilioni 11.9 mwaka 2017/18 sawa asilimia 38 ya bajeti yote.
Mapendekezo
hayo yamewasilishwa hii leo bungeni mjini Dodoma ikiwa ni siku chache
kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
Akiwasilisha mapendekezo hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ametaja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa ni ujenzi wa reli ya kati, kuhuisha shirika la ndege Tanzania na shamba la kilimo na uzalishaji sukari la Mkulazi.
Aidha,
Waziri Dkt. Mpango ametaja changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka
2016/2017 hadi Februari mwaka huu kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi
na hususani kuzingatia matumizi ya mashine ya kielektroniki.
Baadhi
ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi, nje ya ukumbi wa bunge
wamesema serikali imechukua jitihada kubwa katika kuhakikisha
inaondokana na utegemezi kuliko kutegemea fedha kutoka nje.
Post a Comment