TANZIA: Dr. Elly Macha mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA afariki dunia
Dkt Elly Macha (Enzi za uhai wake)
UPDATE
Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kilichotokea katika Hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mpango wa kusafirisha mwili wa Marehemu kuja nchini ikiwa ni pamoja na taratibu za mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu. Kufuatia msiba huu, Mhe. Spika ameahirisha vikao vya kamati vilivyokuwa vinaendelea leo hadi kesho Jumamosi tarehe 1 Aprili, 2017.
Taarifa zaidi juu ya Msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kadri zitakavyopatikana.
''Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi''
AMINA
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
31.03. 2017
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu mkoani Arusha.
"Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha" Amesema Makene
Post a Comment