Lijualikali: Nimepata mateso makali Ukonga
Lijualikali ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online leo mchana baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.
“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.
“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.
Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”
Ameeleza kuwa wakati akifanyiwa vitendo vya kikatili na baadhi askari wa jeshi hilo, asilimia kubwa ya wafugwa walimpokea vizuri na walimpa ushirikiano.
Amesema: “Wafugwa ni watu wazuri, wamekuwa ni walimu wangu, wazazi wangu, washauri wangu na wasiri wangu. Walinipa mashuka.
“Walinipikia chakula pale walipoona nashidwa kula chakula kilichopikwa kwa ajili ya wafugwa. Ambacho ni dagaa waliojaa mchanga na dona tena lililosagwa na mabuzi ya mahindi. Walinisaidia kazi nzito. Ingawa wapo baadhi ambao tulikuwa hautuelewani. Nadhani ni sababu za kisiasa,” ameeleza Lijualikali.
Lijualikali amesema Tanzania bado ina safari ndevu kufikia nchi ambayo inaamini katika uhuru, haki na demokrasia kwa maana halisi. Hivyo amewataka Watanzania kuacha kunyamazia ukiukwaji wa haki dhidi ya raia.
Post a Comment