Kimenukaa Clouds Media..Mfanyakazi Asimamishwa Clouds kwa Kutangaza Habari ya Paul Makonda, TEF Yaitaka Mitandao Iunge Mkono
Bodi
ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo
Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo
vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza
habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Bodi
imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa
msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote
waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa
kwa wiki nzima.
Bodi
inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti,
radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa
Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio
la kuvamia kituo cha Clouds.
Aidha,
Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo
huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum
(Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza
habari zake hatutazichapisha.
Wakati
huo huo, kituo cha Clouds kimepongezwa kwa kumsimamisha kazi mtangazaji
aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.
Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.
Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF
Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017
Post a Comment