Jaji Mkuu Ampa Majukumu Tundu Lissu
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameutaka uongozi mpya wa
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa mpango mkakati
wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ili umoja huo uweze kuchangia
katika kuutekeleza.
Aliyasema hayo jana alipotembelewa na uongozi wa TLS ulioongozwa na Rais wa chama hicho, Tundu Lissu.
Alisema
ni vema kuusoma Mpango Mkakati huo kufahamu ni wapi mahakama inatoka
na wapi inapotaka kuelekea hususan katika suala zima la maboresho ya
huduma ya utoaji haki nchini.
Mpango
Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2010) umegawanyika
katika nguzo kuu tatu ambazo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi
wa rasilimali.
Nyingine
ni upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na kurejesha imani ya jamii na
ushirikishwaji wa wadau na umejikita katika kuboresha huduma za utoaji
haki kwa ujumla.
Naye Rais wa TLS, Tundu Lissu pamoja na mambo mengine alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili mawakili nchini .
Alisema
changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya mahakama kutokuwa na ofisi kwa
ajili ya mawakili, taratibu za usajili wa mawakili, na nyingine.
Akijibu,
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta alisema Mahakama
Kuu inaendelea kufanyia kazi changamoto zote zinazowakabili mawakili.
Mugeta alisema kingine kinachoangaliwa ni kuona uwezekano wa taratibu za malipo kufanyika kwa elektroniki.
Post a Comment